Ni silaha gani muhimu zinazohitajika na Ukraine kuzuia kasi ya Urusi? - BBC News Swahili (2024)

Ni silaha gani muhimu zinazohitajika na Ukraine kuzuia kasi ya Urusi? - BBC News Swahili (1)

Chanzo cha picha, Getty Images

Jeshi la Urusi linaweza kupata mafanikio makubwa katika mashambulizi yanayokuja ikiwa Marekani haitarejesha usaidizi kamili kwa Ukraine. Wanajeshi, wanasiasa na wataalam, wote wa Ukraine na wa Magharibi, wanazungumza sana kuhusu jambo hili. Je, ni aina gani ya uhaba wa silaha na risasi utakaowakumba wanajeshi wa Ukraine iwapo bunge la Marekani litaendelea kuchelewesha upelekaji wa misaada kwa Ukraine?

Kutokana na kukosekana kwa fedha za Marekani kufadhili Ukraine na vikosi vyake vya kijeshi, washirika wengine, hasa wa Ulaya, wanajaribu kusaidia, lakini rasilimali zao hazitoshi.

"Ili kuchukua nafasi kabisa ya msaada wa kijeshi wa Marekani mwaka 2024, Ulaya italazimika kuongeza maradufu kiwango cha sasa na kasi ya upelekaji wa silaha," kwa mujibu wa wachambuzi katika Taasisi ya Kiel.

Ni dhahiri kwamba ni vigumu kuchukua nafasi ya bidhaa za ulinzi za Marekani, hasa ikiwa ni pamoja na silaha ambazo tayari zimetolewa kwa Kyiv.

Ni silaha gani muhimu zinazohitajika na Ukraine kuzuia kasi ya Urusi? - BBC News Swahili (2)

Chanzo cha picha, Getty Images

Je, ni kwa kiasi gani Marekani imetoa silaha kwa Ukraine tangu mwanzo wa uvamizi wa Urusi? Jibu la swali hili liko kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje: "Hadi sasa, Marekani imetoa takriban dola bilioni 44.2 kama msaada wa kijeshi."

Pia kuna orodha ya silaha zilitolewa kwa Ukraine. Sio vitu vyote vilivyoelezewa kwa undani, labda kwa sababu za usiri, lakini habari inayopatikana inatosha kujua usaidizi wa kijeshi wa Marekani.

Hakuna chochote katika orodha ndefu ya silaha za Marekani zinazotolewa kwa Ukraine ambacho washirika wengine wa Kyiv hawana. Kwa hivyo, nchi nyingi zina mifumo ya ulinzi wa anga ya MIM-23 Hawk na makombora yao, na huko Marekani yenyewe yameondolewa kutoka kwa huduma tangu miaka ya mapema ya 2000.

Kwa kuongezea, safu ya ushambuliaji ya nchi za NATO za Ulaya ni tofauti zaidi, na uwezo wa uzalishaji pia ni wa juu. Wana mizinga ya kisasa zaidi na magari ya kivita, na aina zote za silaha, ikiwa ni pamoja na silaha maarufu za "Hymars" , ndege za kivita na zile zisizokuwa na rubani.

Lakini kuwa na kila aina sio kila wakati ni kuzuri, na "ya kisasa zaidi," hii ina maana kwamba hawatatoa nyingi ya hizo.

Ukraine inahitaji kutathmini umuhimu wa kuendelea na vifaa vya Marekani kulingana na vigezo kadhaa.

Suala la kujumuisha silaha

Katika kila kiwango cha silaha, ni vyema kuwa na aina moja ya vifaa badala ya aina mbalimbali tofauti. Kwa mfano, gari la kivita la Marekani la M2 Bradley lina analogi nyingi za kigeni - Puma ya Ujerumani na Marder, Soviet BMP-3 na nyingine. Lakini ikiwa kitengo kina magari ya Bradley, basi kuzibadilisha na vifaa vingine wakati muda wao wa matumizi umefikia mwisho ni suala gumu katika ukarabati na mafunzo, na mwingiliano kwenye uwanja wa vita.

Katika mzozo wa muda mrefu wa kijeshi, vifaa vinavyofanya kazi mbele ya vita huwa vinahitaji kubadilishwa mara kwa mara. Zenye kufaa zaidi mara nyingi kutumika vitani, na kwa hivyo, hufeli mara na mara. Kwa hivyo aina fulani ya silaha inatumika zaidi ndivyo hitaji lake huwa la juu.

Kulingana na kigezo hiki, sasa ni muhimu kwa Ukraine kuendelea kutumia magari ya jeshi la Marekani ya Bradley, howitzers 155-mm na 105-mm, Stryker na magari yasiyopenya risasi ya M113, magari ya kivita na SUV za kila aina, na vile vile vituo vya rada ya kukabiliana na betri.

Ni silaha gani muhimu zinazohitajika na Ukraine kuzuia kasi ya Urusi? - BBC News Swahili (3)

Chanzo cha picha, Getty Images

Silaha zingine zinazotumiwa

Kwa mtazamo wa kwanza, hakuna kitu cha kujadili hapa - haiwezekani kupigana bila risasi na makombora; katika vita unahitaji nyingi, kadiri zinavyoendelea kuwa nyingi ndivyo inavyokuwa bora zaidi.

Swali ni, ni uhaba wa silaha zipi za Marekani unaweza kuipa Ukraine wakati mgumu.

Ni wazi, kwanza kabisa, ukosefu wa zile zinaundwa tu nchini Marekani.

Kwanza, hizi ni silaha ambazo hazitengenezwi au kuhamishwa katika nchi za Ulaya. Marekani haijatia saini mkataba wa kupiga maruf*cku mabomu ya kutawanyika; inaendelea kutumia, kuboresha na kusambaza, ikiwa ni pamoja na kwa Ukraine.

Inajulikana kuwa Pentagon ilipeleka mabomu ya kutawanyika ya M864 milimita 155 kwa Kikosi cha Wanajeshi cha Ukraine.

Pili, makombora ya ardhini na angani. Ndiyo mtengenezaji pekee wa makombora ya ndege ya AIM-120 AMRAAM na AIM-7, pamoja na muundo wake wa majini RIM-7 - Raytheon Corporation.

Makombora ya masafa marefu ya AIM-120 AMRAAM yanatumiwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Marekani-Norway wa NASAMS, unaotumiwa vikosi vya wanajeshi vya Ukraine.

Raytheon pia hutengeneza mifumo ya kudungua ndege ya MIM-104 Patriot, pamoja na makombora yake. Ni kweli inaundwa kwa leseni nchini Japani. Lakini hakuna mahali pengine.

Hii pia ni pamoja makombora ya shabaha ya M30 na makombora ya ATACMS yaliyoundwwa na kampuni ya Marekani ya Lockheed Martin.

Upungufu wa makombora ya kudungua huchanganya sana mapigano dhidi ya shabaha nyingi za anga za ulinzi wa anga wa Ukraine, kama vile makombora ya masafa marefu na ndege za kivita ya balisitiki. Na ukosefu wa makombora ya usahihi wa hali ya juu ya Kikosi cha wanajeshi wa Ukraine hulipa jeshi la Urusi fursa ya kuangazia zaidi kwenye vikosi vikubwa na kuendesha shughuli za kivita.

Ukraine pia inahitaji makombora ya aina yote. Katika hili, Marekani haina ukiritimba, lakini kwa sasa akiba ya makombora na uwezo wa kuongeza uzalishaji wake haraka huko Marekani ni mkubwa zaidi kuliko ile ya washirika wao wa Ulaya.

Silaha za roketi za NATO ni aina moja, kwa hivyo makombora, bila kujali yalitengenezwa Marekani, Canada au Ulaya yanaweza kubadilishwa.

Ni silaha gani muhimu zinazohitajika na Ukraine kuzuia kasi ya Urusi? - BBC News Swahili (4)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kila mtu lazima amtambue mwingine

Ukweli katika maswala ya kijeshi ni kwamba hakuna silaha kuu; mafanikio vitani yanaweza kupatikana tu kupitia mwingiliano wa matawi ya kijeshi na utumiaji wa silaha mbalimbali.

Wataalamu wa kijeshi, haswa, mwangalizi wa kijeshi na kisiasa wa Ukraine wa kikundi cha Upinzani wa Habari Alexander Kovalenko, wanazingatia usawa wa sasa wa utumiaji wa ndege zisizo na rubani na vikosi vya wanajeshi vya Ukraine kwenye mstari wa mbele kwa hasara ya vipengele vingine.

"Katika nyakati zetu ngumu, ndege zisizo na rubani zimepata kazi ya kipekee kama njia muhimu ya kuleta uharibifu. Lakini kwa njia ya ajabu, badala ya kuwa sawa na wengine, walianza kutawala kila mtu, anaandika Kovalenko. - Nilikasirishwa na hawa ambao walitangaza kwamba droni ni bora kuliko mifumo ya kupambana na vifaru. Na walisahau kabisa kuhusu vilipuzi kama sehemu kuu ya kujikinga!

Wanahitaji fedha

Ukraine ina vituo vyake vya uzalishaji, lakini ni wavivu kwa sababu viwanda havina chochote cha kulipa, alisema Waziri wa Viwanda nchini Ukraine Alexander Kamyshin.

Kulingana na yeye, bajeti nzima ya ulinzi ya nchi kwa 2024 ni karibu dola bilioni 40, nyingi ambazo huenda kwa mishahara na malipo kwa wanajeshi, pamoja na gharama ya kudumisha wafanyikazi na vifaa.

“Bado zimesalia dola bilioni 6 kwa ajili ya ununuzi wa silaha. Hiki ndicho kiasi tulichonacho leo katika kandarasi za watengenezaji wetu, hasa wa Ukraine, na hii ni kidogo sana, kwani uwezo wetu wa uzalishaji ni mkubwa mara tatu,” waziri huyo alisema.

Ni silaha gani muhimu zinazohitajika na Ukraine kuzuia kasi ya Urusi? - BBC News Swahili (5)

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanahitaji fedha

Ukraine ina vituo vyake vya uzalishaji, lakini havina kazi kwa sababu viwanda havina chochote cha kulipa, alisema Waziri wa Viwanda nchini Ukraine Alexander Kamyshin.

Kulingana na yeye, bajeti nzima ya ulinzi ya nchi kwa 2024 ni karibu dola bilioni 40, nyingi ambazo huenda kwa mishahara na malipo kwa wanajeshi, pamoja na gharama ya kudumisha wafanyikazi na vifaa.

“Bado zimesalia dola bilioni 6 kwa ajili ya ununuzi wa silaha. Hiki ndicho kiasi tulichonacho leo katika kandarasi za watengenezaji wetu, hasa wa Ukraine, na hii ni kidogo sana, kwani uwezo wetu wa uzalishaji ni mkubwa mara tatu,” waziri huyo alisema.

Ukraine inajadiliana na washirika wa kigeni juu ya ununuzi wa bidhaa za tasnia ya kijeshi ya Ukraine na uhamishaji wa vifaa hivi na silaha kwa vikosi vya wanajeshi vya Ukraine, Kamyshin alisema.

Ni silaha gani muhimu zinazohitajika na Ukraine kuzuia kasi ya Urusi? - BBC News Swahili (2024)
Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Manual Maggio

Last Updated:

Views: 5342

Rating: 4.9 / 5 (49 voted)

Reviews: 80% of readers found this page helpful

Author information

Name: Manual Maggio

Birthday: 1998-01-20

Address: 359 Kelvin Stream, Lake Eldonview, MT 33517-1242

Phone: +577037762465

Job: Product Hospitality Supervisor

Hobby: Gardening, Web surfing, Video gaming, Amateur radio, Flag Football, Reading, Table tennis

Introduction: My name is Manual Maggio, I am a thankful, tender, adventurous, delightful, fantastic, proud, graceful person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.